IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Wakuu wa Kamati za Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

13:54 - February 04, 2024
Habari ID: 3478301
IQNA - Wakati duru ya mwisho ya Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran inakaribia, wakuu wa kamati za maandalizi ya tukio hilo la Qur'ani waliteuliwa.

Katika amri tofauti siku ya Jumamosi, Hamid Majidimehr, ambaye anaongoza Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Jumuiya ya Wakfu na Misaada Iran, aliteua wajumbe wa kamati za maandalizi.

Abbas Salimi aliteuliwa kuwa mkuu wa baraza la kutunga sera na Hujjatul Islam Gholam Reza Adel, Seyed Heydar Mortazavi Shahroudi, Abbas Lohrasbi, Mehdi Taheri Moqaddam, Hujjatul Islam Shozab Shiri, Seyed Mostafa Malihi, Hujjatul Islam Rafie , na Mohammad Taqi Mirzajani walitajwa kuwa wenyeviti wa kamati tofauti.

Pia, Hamid Reza Mostafid na Mahboubeh Kateb waliteuliwa kuwa wakuu wa majopo ya majaji katika sehemu za wanaume na wanawake, mtawalia.

Kwa mujibu wa Majidmehr, hatua ya fainali itaanza Alhamisi, Februari 15, mkesha wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Sajjad (AS) na sherehe ya kufungua itafanyika Jumatano, Februari 21, wakati wa sherehe za Sha’abaniyah.

Kwa upande wa wanaume, Hadi Esfidani ataiwakilish Iran katika kipengele cha usomaji wa Qur'ani akiwa na Omid Reza Rahimi naye Mohammad Poursina akiwakilisha Iran katika kuhifadhi na Tareel.

Wawakilishi wa Iran katika sehemu ya wanawake ni Roya Fazaeli katika kuhifadhi Qur'ani nzima na Adeleh Sheikhi huko Tarteel.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hafla ya kila mwaka ambayo huwavutia wasomaji na kuhifadhi Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani, na kukuza urafiki na kati ya nchi za Kiislamu.

Duru ya awali ya shindano hilo ilianza mwishoni mwa Desemba, wakati jopo la majaji lilipotathmini maonyesho yaliyorekodiwa ya washiriki 138 kutoka nchi 64.

4197563

Habari zinazohusiana
captcha