IQNA

Mashidano ya Qur'ani

Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran: Muhtasari wa Siku ya Pili

11:42 - February 18, 2024
Habari ID: 3478371
IQNA - Siku ya pili ya Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ilishuhudia washindani 25 kutoka nchi mbalimbali wakionyesha ustadi wao wa kusoma na kuhifadhi kitabu kitakatifu huko Tehran siku ya Jumamosi.

Siku hiyo pia iliadhimishwa siku ya kwanza ya mashindano ya wanawake, na vilevile siku ya pili ya awamu ya 8 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanafunzi wa shule za ulimwengu wa Kiislamu, ambayo yanafanyika sambamba na Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.
Makari saba wa kike na 10 wa kiume na wahifadhi walishindana katika kategoria kuu za usomaji wa Qur'ani (kwa wanaume) na kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tarteel (kwa wanaume na wanawake).
Visomo vya washindani katika kategoria ya usomaji wa Tahqiq vinapatikana hapa chini. Mashindano hayo yaliyoanza siku ya Alkhamisi yamewavutia wapenzi wa Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwemo viongozi na watu mashuhuri wa Iran. Zaidi ya nchi 110 zilijiandikisha kwa shindano hilo, lakini ni wahitimu 69 tu kutoka nchi 40 waliofanikiwa kuingia katika duru ya mwisho baada ya mchakato mkali wa mchujo.
Mashindano hayo yataendelea hadi Jumanne, Februari 20, na washindi watatunukiwa katika hafla ya kufunga Jumatano, Februari 21. Hafla hiyo ya kila mwaka, inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

 
 
4200425
Habari zinazohusiana
captcha