IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

Qari wa Algeria apongeza kauli mbiu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

20:39 - February 20, 2024
Habari ID: 3478383
IQNA - Qari wa Algeria anayeshiriki katika Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran apongeza kauli mbiu ya mwaka huu ya tukio hilo adhimu la Qur'ani.

Akizungumza na IQNA, Ustadh Abdullah Mazuzi aliwashukuru waandaaji kwa kuchagua “Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Muqawama (Mapambano ya Kiisalmu" kuwa kauli mbiu ya mashindano hayo.

Ameieleza kuwa ni yenye maana kubwa kama vile Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinawaleta Waislamu wote pamoja na kuwaunganisha, huku akibainisha Aya ya 103 ya Surah Al Imran: “Na shikamaneni na Kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msitawanyike.

Mazuzi amegusia nafasi ya matukio hayo ya Qur'ani katika kuimarisha umoja wa Kiislamu na kusema kwa kuendeleza kuijua Qur'ani na mafundisho yake, yanachangia umoja wa Umma wa Kiislamu.

Amesema huo ni ushiriki wake wa kwanza katika mashindano ya Qur'ani ya Iran, akipongeza mipango mizuri na kiwango cha juu cha washindani.

Alipoulizwa kuhusu shughuli za Qur'ani nchini mwake, qari huyo ambaye pia ni hhafidh wa Qur'ani nzima alisema watu nchini Algeria wanawapeleka watoto wao katika shule za Qur'ani na misikitini ili kujifunza Kitabu hicho kitakatifu tangu wakiwa wadogo.

Alisema yeye mwenyewe alianza kujifunza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri mdogo na aliweza kuhifadhi Quran nzima akiwa na umri wa miaka 14.

Kisha akajifunza ujuzi wa kusoma Qur'ani pamoja na masomo yake ya shule.

Kwingineko katika maelezo yake, Mazuzi alisema amejifunza mengi kutoka kwa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri na kwamba anamheshimu na kumpenda Mohammad Sidiq Minshawi.

Aidha anawatakia mwisho wa mateso watu wa Ukanda wa Gaza, ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya mauaji ya halaiki ya Israel kwa muda wa miezi mitano na kuwaombea ushindi.

Fainali ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran  ilizinduliwa mjini Tehran siku ya Alhamisi na itaendelea hadi Februari 21.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji 69 kutoka nchi 44 wanashindana katika fainali katika kategoria kuu za usomaji wa Qur'ani (kwa wanaume) na kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tarteel (kwa wanaume na wanawake).

Hafla hiyo ya kila mwaka, inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

3487254

Habari zinazohusiana
captcha