IQNA

Jinai za Israel

Idadi ya mashahidi huko Gaza imepindukia 33,500, Israel yaendeleza mauaji ya kimbari

11:25 - April 12, 2024
Habari ID: 3478672
IQNA-Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza imefikia 33,545 huku utawala huo katili ukiendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.

Kwa mujibu wa IQNA, Wizara ya Afya ya Palestina huko Ghaza ilitangaza Alhamisi kwamba, idadi ya mashahidi wa vita vya Wazayuni huko Ghaza tangu tarehe 7 Oktoba imeongezeka na kufikia 33,545.

Kulingana na ripoti hii, idadi ya waliojeruhiwa imefikia watu elfu 76 na 94.

Aidha ripoti hiyo imebaini kkuwa, zaidi ya watu 7,000 bado hawajulikani walipo, wengi wakiaminika kuwa chini ya vifusi, na juhudi za kuwaondoa bado zinaendelea.

Asilimia 73 ya mashahidi na waliojeruhiwa katika vita huko Gaza ni wanawake na watoto. Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesisitiza kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni na askari wa utawala huo wanapotosha na wanaichezea misingi ya sheria za kimataifa ili kuhalalisha ukatili na uchokozi wao. Francesca Albanese, ametoa wito wa kupigwa marufuku uuzaji wa silaha kwa Israel na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi utawala huo dhalimu na ghasibu.

Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina, na kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu mbele ya jinai za Israel zimepelekea kuendelezwa mauaji ya wanawake na watoto Palestina yanayofanywa na utawala huo. 

4209930

Habari zinazohusiana
captcha