IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ya kitengo cha wanawake yamalizika

20:06 - February 20, 2024
Habari ID: 3478380
IQNA - Siku ya tatu ya kitengo cha wanawake katika Awamu ya 40 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran ilishuhudia wahifadhi kutoka nchi 11 waliofaulu.

Washindani kutoka Senegal, Afghanistan, Iran, Kanada, Nigeria, Oman, Marekani, Sri Lanka, Indonesia, Pakistan na Singapore walionyesha vipaji na ujuzi wao wa Qur'ani Jumatatu, siku ya mwisho ya mashindano katika sehemu hii.
Sehemu ya wanaume katika kategoria za kusoma na kuhifadhi  imeendelea leo Jumanne.
Fainali ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran  ilizinduliwa mjini Tehran siku ya Alhamisi na itaendelea hadi Februari 21.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji 69 kutoka nchi 44 wanashindana katika fainali katika kategoria kuu za usomaji wa Qur'ani (kwa wanaume) na kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tarteel (kwa wanaume na wanawake).

Hafla hiyo ya kila mwaka, inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

3487263

Habari zinazohusiana
captcha