IQNA

Watetezi wa Palestina

Rais wa Iran: Kadhia ya Palestina sasa ni kadhia ya kwanza ya jamii ya mwanadamu

20:09 - January 14, 2024
Habari ID: 3478198
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran amesema kuwa, kadhia ya Palestina imegeuka na kuwa kadhia ya kwanza ya jamii ya mwanadamu ulimwenguni.

Ebrahim Raisi amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika Kongamano la Kimataifa la Kimbunga cha al-Aqsa na Kuamsha Hisia za Ubinadamu za Walimwengu na kueleza kwamba, Imam Khomeini (RA), muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa, Palestina ni suala la kwanza la ulimwengu wa Kiislamu, na kukombolewa Quds (Jerusalem) ni jambo la kipaumbele katika ulimwengu wa Kiislamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, muqawama, mapambano na kusimama kidete mkkabala wa adui Israel ndio suluhisho la kadhia ya Palestina na kuongeza kuwa: "Ikiwa mkondo wa kidhalimu hauelewi lugha ya mantiki na mazungumzo, basi mantiki pekee ni muqawama na mapambano."

Soma zaidi

Iran kuandaa Kongamano la Kimataifa la Kuiunga Mkono Gaza

Kadhalilika Sayyid Ebrahiim Raisi amesema, katika sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, suala la kuunga mkono kadhia ya Palestina na makundi ya muqawama na mapambano ni miongoni mwa ajenda za taifa hili.

Aidha amehoji kwa kusema, hivi tunaweza kuwapuuza watu wanaodhulumiwa zaidi duniani? Ni lazima kumuunga mkono na kumtetea mtu ambaye anasimama na kujitetea yeye, dini na familia yake.

Aiidha Rais wa Jamahuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kongamano hilo la Kimataifa la Kimbunga cha al-Aqsa na Kuamsha Hisia za Ubinadamu za Walimwengu kwamba, uvamizi wa Israel na ukaliaji wake kimabavu ardhi za Wapalestina unapaswa kukomeshwa na wakati huo huo mvamizi aadhibiwe na kulipa fidia.

Vilevile amesema, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia wa Israel hakudhamini kwa namna yoyote ile usalama wa Asia Magharibi wala wa utawala haramu wa Israel.

3486804 

captcha