IQNA

Jinai za Israel

Utawala katili wa Israel kufikishwa kizimbani ICJ wiki ijayo

16:39 - January 04, 2024
Habari ID: 3478147
IQNA-Mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu tuhuma za mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza kuanza kusikilizwa wiki ijayo.

Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) imetangaza kwamba, itafanya vikao vya wazi tarehe 11 na 12 Januari kwa ajili ya kusikkiliza shauuri la mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Israel kuhusu vita dhidi ya Gaza.

Kufuatia kuendelea jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, wiki iliyopita Afrika Kusini iliushtaki rasmi utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu huko The Haque.  Mastaka muhimu ya Afrika Kusini ni jinai za kivita, mauaji ya kizazi na kikabila huko Gaza na katika maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Hatua hiyo ya Afrika Kusini imechukuliwa huku Wazayuni wakiendeleza kwa miezi mitatu sasa mashambulizi ya kinyama ya mabomu dhidi ya raia wa kawaida huko Gaza, hasa wanawake na watoto.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi za Kiafrika ambazo tokea yalipoanza mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Wapalestina zimetoa radiamali na kulaani hatua hizo za kinyama za Wazayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Gaza. Aghalabu ya nchi hizo ambazo zilitawaliwa kwa miaka mingi na nchi za Magharibi na kukumbana na ukoloni, unyonyaji na ubaguzi wa rangi sambamba na kulaani jinai za Israel, zimetaka kukomeshwa ukatili unaofanyiwa wananchi wanaozingirwa wa Gaza

Afrika Kusini, ikiwa ni nchi ambayo ilikumbana na mateso ya utawala wa kibaguzi kwa miongo kadhaa na inayoongoza  mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani, ilianzisha juhudi za kukomesha mauaji ya Wapalestina tangu mwanzoni mwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Gaza kufuatia Kimbunga cha Al-Aqsa tarehe 7 Oktoba.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza Alhamisi kuwa, takwimu za karibuni kabisa za idadi ya Wapalestiina waliouawa shahidi tangu utawala haramu wa Israel uanzishe hujuma yake ya mauaji ya kimbari huko Gaza imefikia 22,313.

Aidha kwa mujibu wa tangazo hilo, Wapalestina 57,296 wamejeruhiwa hadi sasa huku hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ikiripotiiwa kuwa mbaya.

4191987

Habari zinazohusiana
captcha