IQNA

Tauhidi katika Qur'ani Tukufu/1

Nukta kuhusu mwanzo na mwisho wa Dunia

18:27 - November 08, 2022
Habari ID: 3476055
TEHRAN (IQNA) – Suala la mwanzo na mwisho wa dunia ni miongoni mwa maswali muhimu yaliyo mbele ya wanadamu na namna wanavyoyajibu huwa na athari kubwa katika maisha na hatima ya watu binafsi.

Hujjatul Islam Mohammad Ali Khosravi, mtafiti katika nyanja ya dini, anazungumzia mtazamo wa ulimwengu, falsafa ya majira ya kuchipua, ufufuo baada ya kifo, na swali la kawaida juu ya mwanzo na mwisho wa dunia. Huu hapa ni muhtasari wa kikao chake cha kwanza:

Mojawapo ya maswali ambayo kila mwanadamu, ama mwamini au asiyeamini, anajaribu kujibu ni kuhusu mwanzo na mwisho wa dunia. Tunaweza kuuliza: “Nimetoka wapi? Sababu ilikuwa nini? Na ninaelekea wapi?"

Watu walioshindwa kujibu swali hili wameielezea dunia kuwa ni kitabu cha zamani ambacho kimepoteza ukurasa wake wa kwanza na wa mwisho; hii ina maana kwamba jina la mwandishi wala mwisho wa hadithi haipatikani.

Moja ya misheni kuu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni kujibu maswali haya na Qur'ani Tukufu  pia inazingatia mada hii kuelezea chanzo na hatima ya wanadamu. Hata hivyo, si Mitume wala Qur'ani inayojishughulisha na falsafa ya kujibu maswali. Qur'ani Tukufu imewajibu wanadamu kwa kutumia maelezo yanayoshikika na yaliyo wazi. Aya ya 7 na 8 za Sura Qaf zinasema: “Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. "

Aya zinataja sababu mbili za ukuaji wa mimea: mwamko na ukumbusho. Aya inayofuata ya Sura inasema: “Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa. ” Kwa hiyo aya hizi zinaeleza mchakato wa ukuaji.

Na katika Aya ya 11, mavuno yametajwa kuwa kuwa riziki kwa waja. "Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji.”

Haya yanaonyesha kwamba hakuna haja ya mijadala ya kifalsafa; mtu anahitaji kutazama kwa kina zaidi katika chemchemi ili kumwamini Mwenyezi Mungu na kujibu maswali kuhusu Akhera.

3481168

captcha