IQNA

Umoja wa Kiislamu

Utawala wa Kizayuni unaleta mifarakano miongoni mwa mataifa ya Kiislamu

21:54 - August 20, 2022
Habari ID: 3475651
TEHRAN (IQNA) – Khatibu wa Kisunni wa Iraq anasema utawala wa Kizayuni wa Israel unapanda mbegu za mifarakano kati ya mataifa ya Kiislamu ili kufikia malengo yake.

Akizungumza na IQNA, Sheikh Abdul-Amir al-Kilani, Imamu wa Msikiti wa al-Aboud mjini Baghdad ametoa mawazo yake kuhusu utawala wa Israel na vilevile umoja baina ya Waislamu.

Utawala wa Tel Aviv unatumia Marekani kushinikiza mataifa mengine kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya tawala katika eneo la Asia Magharibi tayari zimechukua mkondo huo, amebaini.

Mnamo mwaka wa 2020, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain zilitia saini mikataba ya Marekani na Israel ili kuanzisha uhusiano wa kawiada na utawala huo unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.

Baada ya hapoi Sudan na Morocco, zilifuata nyayo hizo hizo pamoja na kuwa wananchi walipinga vikali uamuzi huo.

Makubaliano hayo yanayoitwa Abraham yamekosolewa sana na Wapalestina pamoja na mataifa na watetezi wa haki za binadamu kote ulimwenguni, haswa ndani ya ulimwengu wa Kiislamu.

Wazayuni wanatekeleza ndoto zao za Nile hadi Euphrates huku utawala huo wa Tel Aviv ukijaribu kupanua ushawishi wake katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijeshi, alibainisha mwanazuoni huyo wa Kisunni.

Njia pekee ya kuikomboa Palestina ni kupitia mapambano, alisema, akiongeza kuwa wale wote wanaoweza kuchukua silaha wanapaswa kufanya hivyo.

Kwingineko, aliashiria ulazima wa umoja wa Waislamu mbele ya adui Mzayuni,

Sheikh Al-Kilani alisema umoja unapatikana ikiwa Waislamu watazingatia zaidi maana ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu na wajiweka mbali na kuzozana kutokana na tofauti ndogo ndogo.

captcha