TEHRAN (IQNA)- Hivi karibuni klipu imesambaa katika mitandao ya kijamii kuhus Qarii wa Misri, Marhum Sheikh Antar Saeed Musallam akisoma dua kabla ya kuanza qiraa ya Qur'ani Tukufu.
Sheikh Musallam ni Qarii maarufu wa Qur'ani wa Misri aliyezaliwa mwaka 1936 mjini Qotour katika Jimbo la Gharbia nchini humo. Alihifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka 8 na aliaga dunia Septemba 2, 2002.