IQNA

Qarii wa Lebanon akisoma Sura Aal Imran kwa sauti yenye mvuto

TEHRAN (IQNA)-Klipu ya qarii maarufu wa Lebanon Ustadh Hamza Mon’em akisema baadhi ya aya za Sura Aal Imran katika Qur'ani Tukufu imesambaa katika mitandao ya kijamii.

Ustadh Mon’em, ambaye ni qarii wa kimataifa na mhadhiri wa sayansi za Qur'ani, amesoma aya za 126 hadi 129 za Sura Aal Imran katika kikao cha Jumuiya ya Qur'ani nchini Lebanon.