IQNA

Katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria

Rais Raisi: Iran inataka kuboresha uhusiano na mataifa ya Afrika

20:02 - August 06, 2021
Habari ID: 3474164
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran na Nigeria zimekuwa zishikishirikiana vyema katika nyanja mbalimbali.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo mapema leo katika mazungumzo yake na Zubairu Dada Waziri Mshauri wa Mambo ya Nje wa Nigeria aliyeko safarini mjini Tehran.

Amesema, kwa kuzingatia uwezo mzuri wa nchi mbili Iran iko tayari kuchukua hatua kubwa na za dhati kuboresha zaidi na kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili.  

Sayyid Ebrahim Raisi ameashiria namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyo na azma thabiti ya kustawisha mahusiano na nchi za Kiafrika na kuongeza kuwa: Viongozi wa Nigeria pia wanapaswa kufanye juhudi za kuondoa vizuizi vinavyoweza kukwamisha kazi ya kupanuliwa uhusiano kati ya nchi mbili.

Kwa upande wake Zubairu Dada Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria  amesema, uhusiano kati ya nchi mbili ni wa kirafiki na mzuri na kwamba anarataji kuwa kiwango cha ushirikiano wa pande mbili kitaimarishwa zaidi na zaidi katika kipindi cha sasa. 

130356

Kishikizo: iran raisi nigeria africa
captcha