IQNA

Mtoto Mwislamu apigwa risasi Uingereza

7:54 - May 18, 2015
Habari ID: 3304654
Mtoto Mwislamu mwenye umri wa miaka miwili amepigwa risasi na kuumizwa vibaya kichwani katika mji wa Bradford nchini Uingereza.

Taarifa zinasema kuwa msichana huyo mdogo alipigwa risasi na matu asiyejulikana wakati akiwa ameandamana na mama yake.
Akizungumza na waandishi habari, mama ya msichana huyo, Noor Nahar amesema ana wasi wasi mkubwa kuwa yamkini watoto wengine wakahujumiwa iwapo aliyetekeleza uhalifu huo hatiwi mbaroni. Mwanamke huyo Mwislamu mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akielekea kumchukua mwanae shuleni wakati hujuma hiyo ilipojiri siku ya Alkhamisi. Msichana aliyepigwa risasi, Noorsadia Akhter, ameachwa na jeraha kichwani baada ya hujuma hiyo. Alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji na kisha kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Familia ya Nahar ni ya Waislamu wa kaumu ya Rohingya kutoka Myanmar ambao waliwasili Uingereza miaka sita iliyopita wakikimbia dhulma katika nchi yao.  Kuna Waislamu karibu milioni mbili nchini Uingereza na kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu kumeshuhudiwa kuongezeka kwa karibu asilimia 10 hujuma dhidi ya wanawake Waislamu nchini humo katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.../mh

3304394

captcha