IQNA

Nafasi ya Imam Sadiq (AS) katika Maendeleo, na Mizunguko ya Ukuzaji wa Elimu

11:47 - October 12, 2023
Habari ID: 3477719
TEHRAN (IQNA) – Imam Sadiq (AS) aligawanya sayansi za Kiislamu katika nyanja mbalimbali kama vile Fiqhi (sheria), teolojia, Hadith, tafsiri ya Qu’rani Tukufu, n.k, na kuanzisha mkondo wa maendeleo ya elimu.

Haya ni kwa mujibu wa Mohammad Sadeq Elmi, akizungumza na IQNA kuhusu nafasi ya Imam Sadiq (AS) katika ukuzaji wa elimu, Zifuatazo ni nukuu za maneno yake;

Maimamu wanne wa kwanza wa Shia (AS) walikumbana na vikwazo na mashinikizo, lakini mashinikizo na vizuizi hivi vilipungua wakati wa Imam Baqir (AS) na Imam Sadiq (AS), Kwa hiyo baada ya uimamu wa Imam Baqir (AS) fursa ya pekee, kutoka katika nyanja ya kisiasa, ilionekana kwa Mashia na wakati huu, Imam Sadiq (AS) aliwafunza wanafunzi wengi katika nyanja tofauti za elimu. Aliwazoeza wanafunzi wapatao 4,000 katika nyanja mbalimbali, Miongoni mwao walikuwa Hisham katika theolojia na Zararah na Muhammad ibn Moslim katika Hadith.

Kabla ya Imamu Sadiq (AS), nyanja za elimu zilichanganyika na hapakuwa na uainishaji wa hizo,Haikuwa wazi ni nani ni mwalimu wa Hadithi,  Tafsiri ya Qur'ani Tukufu, theolojia, n.k. Ainisho la sayansi, ambalo tunaliita maendeleo ya elimu hivi leo, lilifanyika katika zama za Imam Sadiq (AS) na chuo kikuu cha sayansi za Kiislamu iligawanywa katika fani mbalimbali kama vile Fiqhi, teolojia, Hadith, Tafsir, n.k.

Imamu Sadiq (AS): Kielelezo cha Ulimwengu Katika Elimu

Jabir ibn Hayyan alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Imam Sadiq (AS), Aliandika zaidi ya risala 1,200 na makala katika nyanja za fizikia, kemia na sayansi nyinginezo.

Ibn Nadim alikuwa mwanafunzi mwingine wa Imam (AS) ambaye aliainisha sayansi katika kazi yake maarufu ya Al-Fihrist.,Katika kitabu hiki, Ibn Nadim anasema kila mara Jabir ibn Hayyan alipozungumza kuhusu masuala ya kisayansi na kielimu alikuwa akisema aliyasikia kutoka kwa Imam Sadiq (AS).

Abu Hanifah, ambaye anajulikana miongoni mwa madhehebu nne za Kisunni kama ,Imam Azam pia alikuwa mwanafunzi wa Imam wa sita wa Shia ,Abu Hanifah pia alikuwa ni mwalimu wa maimamu wengine wa shule za Sunni na, kwa hivyo, maimamu hawa pia kwa njia isiyo ya moja kwa moja walikuwa wanafunzi wa Imamu Sadiq (AS).

Abu Hanfah mara kwa mara alikuwa akisema; Kama isingekuwa miaka hiyo miwili ya uanafunzi chini ya Imamu Sadiq (AS), Nu’man Abu Hanifa angeangamia.

Kufundishwa  kwa wanafunzi wengi sana na kuwaalika kwenye midahalo na ukweli kwamba Abu Hanifah na watu wengine wakubwa wa Kisunni wamesimulia Hadithi kutoka kwa Imam Sadiq (AS) zote ni dalili za uhusiano mzuri na wa kirafiki wa Imam (AS) na Masunni.

Kwa ujumla, kuna Hadiyth nyingi kutoka kwa Imamu Sadiq (AS) kuhusu uhusiano wa karibu na mzuri na Masunni.

Kitabu cha The Mastermind of the Shia World, kilichoandikwa kuhusu Imam Sadiq (AS) na makumi ya wanazuoni wasio Waislamu wa Magharibi, kinajumuisha makala zinazozungumzia mafundisho ya kisayansi ya Imam Sadiq (AS) ambazo ziliwasilishwa katika semina nchini Ufaransa.Ninapendekeza kusoma kitabu hiki, ambacho kimeidhinishwa na mtu mashuhuri wa Shia Imam Musa Sadr.

 

3485525

 

 

Kishikizo: Imam Sadiq ahlul bait
captcha