IQNA

Shakhsia katika Qur'ani Tukufu /39

Yahya; Nabii aliyemthibitisha Nabii Isa

13:51 - May 01, 2023
Habari ID: 3476941
TEHRAN (IQNA) – Yahya -Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-(AS)-, anayejulikana pia kama, alikuwa mtoto wa Zakariya (AS) na aliteuliwa kuwa utume tangu utotoni.

Alichukua nafasi kubwa katika kuunga mkono na kuendeleza utume wa Nabii Isa (AS).

Yahya alikuwa miongoni mwa Mitume wa Bani Isra’il. Kuna maoni tofauti kuhusiana na jina lake, ambalo linamaanisha 'yule anayeishi na ambaye hajafa'. Baadhi, kwa mfano, wanasema aliitwa Yayha kwa sababu Mungu aliwafadhili wazazi wake kwa kuzaliwa kwake ingawa mama yake alikuwa ameonekana kuwa tasa.

Yahya aliweza kupata taufiki na kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu utotoni. Mungu alimpa hekima na busara nyingi katika umri mdogo ili aweze kuteuliwa utume.

Katika Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anasema kuhusu Yahya: “Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto. Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mcha mungu.” (Surah Maryam, Aya ya 12-13)

 Pia Nabii Yahya (AS) anatambulishwa kama aliyeimuidhinisha Nabii Isa (AS) ambaye Wakristo wanamuita Yesu.

Wakristo humwita Yahyah, Yohana Mbatizaji kwani yaye ndiya aliyembatiza Nabii Isa. Yahya alieneza dini ya Musa (AS) na  Isa (AS). Katika riwaya za kihistoria, Yahya, ambaye alikuwa na umri wa miezi sita au miaka mitatu zaidi kuliko Isa, ametajwa kuwa mtu wa kwanza aliyemwidhinisha Isa. Kwa sababu Yahya alijulikana miongoni mwa watu kwa utakasifu wake, uidhinishaji wake ulikuwa mzuri sana kwa watu kuukubali wito wa Isa.

Katika vyanzo vya kihistoria na kidini, Yahya anajulikana kwa mambo makuu matano, yaani, kumwamini Isa, ubora wa maarifa na matendo, ukarimu, uchaji Mungu, na adhama. Inasemekana alilia sana na kuvaa nguo zilizotengenezwa kwa pamba.

Jina lake limetajwa mara tano katika Sura nne za Qur'ani Tukufu. Hadithi ya kuzaliwa kwake na baadhi ya sifa zake zimetajwa katika Surah Maryam. Mungu anasema hivi kumhusu: “Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.” (Aya ya 15 ya Surah Maryam)

Kuna hadithi kuhusu Yahya katika Biblia ambazo zinafanana kabisa na zile za Qur'ani Tukufu. Hadithi kuhusu Zakariya kupokea habari za kuzaliwa kwake inakuja katika Injili ya Luka. Mambo makuu kuhusu Yahya yanayotajwa katika Biblia ni pamoja na kumwidhinisha Yesu, kutangaza dini yake na kumbatiza.

Yahya, kama baba yake Zakariya, aliuawa. Wakati fulani mfalme wa Bani Israil alimpenda mmoja wa jamaa zake na alitaka kumuoa lakini Yahya alipinga. Msichana huyo alisema atakubali kuolewa na mfalme ikiwa atamuua Yahya na kupeleka kichwa chake. Mfalme aliamuru kuuawa kwake na akapeleka kichwa cha Yahya kwake katika sahani ya dhahabu.

Kuna maeneo tofauti ambayo yanasemekana kuwa amezikwa Yahya, na maarufu zaidi ni Msikiti wa Umayyad huko Damascus. Mwili wake unasemekana kuzikwa hapo huku kichwa chake kikizikwa katika mtaa wa al-Zabadani mjini humo.

Kishikizo: nabii yahya nabii isa
captcha