Haya ni kwa mujibu wa Mohsen Davari, gavana wa Mashhad, ambaye alisema siku ya Jumamosi kwamba makao makuu yameanzishwa ili kuratibu juhudi za kuwahudumia mahujaji.
Mahujaji wote watakaribishwa katika sehemu za kuingilia iwe wanasafiri kwa nchi kavu, kwa ndege au kwa gari moshi, alibainisha.
Afisa huyo aliongeza kuwa usimamizi wa hoteli na kituo cha malazi umeimarishwa ili kuhakikisha watatoa huduma zinazostahiki.
Mashhad ni makao ya kaburi takatifu au Haram ya Imam Ridha (AS), Imam wa 8 wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia na mjukuu wa Mtume Muhammad SAW. Ni moja ya vituo vya Ziyara vinavyotembelewa zaidi ulimwenguni.
Makumi ya mamilioni ya wafanyaziyar kutoka kote Iran pamoja na nchi nyingine hutembelea mji huo mtakatifu kila mwaka.
Ni mojawapo ya maeneo yanayopendwa sana na Wairani wakati wa likizo ya Nowruz ambayo inaashiria mwanzo wa Mwaka Mpya wa Hijria Shamsiya.
4125880