IQNA

Umoja wa Kiislamu

Mufti wa Kazakhstan asisitiza nafasi ya wanazuoni katika kuimarisha Umoja wa Waislamu

13:03 - February 16, 2023
Habari ID: 3476570
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Nauryzbai Haji Taganuly, Mufti Mkuu wa Jamhuri ya Kazakhstan, amsema ni wajibu kwa wanazuoni wa Kiislamu kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha umoja katika Umma wa Kiislamu.

Aliyasema hayo jana Jumatano wakati akihutubia katika Mkutano wa Pili wa Umoja wa Kiislamu wa Kieneo katika Mkoa wa Golestan, kaskazini mwa Iran.

Mwanazuoni huyo mwandamizi ameongeza kuwa, Umma wa Kiislamu unapaswa kulinda na kuimarisha umoja na mshikamano wake kwa ajili ya kupata baraka za Mwenyezi Mungu.

Aidha alipongeza mkutano huo wa kikanda wa umoja wa Kiislamu na kusema tukio hilo linachangia kuimarisha ushirikiano kati ya Waislamu.

Alilishukuru Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (WFPIST) kwa kuandaa mkutano huo na kusema mikusanyiko ya aina hiyo ni mahali pa wasomi na wanafikra wa Kiislamu kukutana na kubadilishana mawazo.

Kwingineko katika matamshi yake, Mufti Mkuu wa Jamhuri ya Kazakhstan ameashiria taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu na kwa nchi yake.

Mkutano huo ulianza huko Gorgan, mji mkuu wa Mkoa wa Golestan, siku ya Jumanne, na utahitimishwa leo.

Mwanazuoni 20 wa madhehebu za Shia na Sunni kutoka Iran, Russia, Kazakhstan, Uzbekistan, Turkmenistan na Kyrgyzstan wamehutubia kikao hicho cha siku mbili.

‘Fikra za Shahidi Soleimani; Kielelezo cha Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na Kufikiwa Ustaarabu Mpya wa Kiislamu’ ndio mada kuu ya mkutano huo.

Pamoja na mambo mengine, lengo lake ni kuendeleza utamaduni wa kukurubisha madehehebu za Kiislamu, kufafanua umuhimu kukurubisha madhehebu za Kiislamu, na kutambulisha harakati ya kukurubisha madhehebu za Kiislamu kama moja ya mafanikio makuu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

584170

captcha