Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 33 ametangaza kuachana na Ukristo na kuikumbatia dini tukufu ya Kiislamu katika halfa iliyosimamiwa na Idara ya Kimataifa ya Harama ya Imam Ridha AS mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.
Mwanamke hiyo akiwa katiak eneo hilo takatifu ametamka shahda mbili na kusilimu baada ya mashauriano na mtaalamu wa masuala ya Kiislamu.
Akizungumza kuhusu sababu ya kusilimu amesema: “Nimeuchagua Uislamu baada ya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Aidha nimejifunza kutoka baada ya binamu zangu na marafiki Waislamu.”
Baada ya kusilimu, mwanamke huyo ametunukiwa vitabu vya Kiislamu na pia zawadi za kiutamaduni.
https://iqna.ir/en/news/3478225/