IQNA

IQNA yaandaa kikao cha kimataifa cha intaneti kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu

17:31 - February 06, 2022
Habari ID: 3474898
Shirika la Habari za Qur'ani Tukufu la Kimataifa (IQNA) litafanya kongamano la kimataifa kupitia intaneti kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kongamano hilo ambalo limepewa anuani ya “Mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Mapambano (Muqawama) Duniani”, limepangwa kufanywa Jumanne, Februari 8.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Manouchehr Mottaki atahutubia hafla hiyo mubashara moja kwa moja.

Wazungumzaji wengine ni naibu katibu mkuu wa Hezbollah Sheikh Naim Qassim, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Iraq ya al-Nujaba Nasr al-Shammari, na mwanaharakati wa kisiasa wa Yemen Sayed Sadegh Al-Sharafi.

Mtandao huo utafanyika kati ya saa mbili asubuhi hadi saa nne na nusu asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na kutangazwa moja kwa moja kutoka kwa kiungo hiki na pia akaunti ya Instagram ya IQNA.

IQNA to Host Int’l Webinar about Islamic Revolution

4034211

captcha