Gavana wa Jenin akisema kuwa, mabarobaro hao wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi alfajiri ya leo Jumatatu katika kambi ya wakimbizi ya Jenin huko Ukingo wa Magharibi.
Amesema utawala huo wa Kizayuni umezuilia maiti mbili za vijana hao waliouawa. Afisa huyo wa Jenin amewataja vijana watatu miongoni mwa wanne waliouawa kuwa ni Saleh al-Ammar, Raed Abu Seif, na Nour Jarrar.
Kwa mujibu wa takwimu, kuna walowezi wa Kizayuni wapatao 650,000 wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds (Jerusalem) Mashariki.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Ukingo wa Magharibi na Quds ni maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na hivyo ujenzi wa vitongoji ni kinyume cha sheria.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha maazimio kadhaa ya kuutaka utawala wa Kizayuni uondoke katika ardhi za Palestina ambazo unazikalia kwa mabavu.