IQNA

OIC: Mgogoro wa Afghanistan usitishwe kwa mazungumzo

21:06 - August 15, 2021
Habari ID: 3474192
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa wito kwa wahusika wote wa mgogoro Afghanistan kuachana na ghasia na kutatia matatizo yaliyopo kwa njia ya mazungumzo.

Sekretarieti ya OIC katika taarifa ilisema mazungumzo ni njia ya kuelekea amani na usalama nchini Afghanistan.

OIC imehimiza pande zinazopigana kusitisha mizozo, kuanza mazungumzo na kuelekea katika usitishaji mapigano ya kudumu.

Taarifa hiyo ilionyesha utayarifu wa OIC kusaidia juhudi za kuanzisha amani na utulivu nchini Afghanistan.

Ripoti za hivi punde zinaonyesha kuwa Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, sasa uko mikononi mwa Taliban na Rais Ashraf Ghani ametoroka nchi.

Hivi karibuni pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema Huu ni wakati wa Afghanistan kuacha mashambulizi, huu ni wakati wa kuanza mazungumzo makini na huu ni wakati wa kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyokoma.

Guterres amekumbusha kuwa ni suluhu ya kisiasa pekee inayoongozwa na waafghanistan ndio inaweza kutoa hakikisho la amani na kwamba Umoja wa Mataifa kwa upande wake umeazimia kuchangia katika suluhu hiyo, na kusongesha haki za wananchi wa Afghanistan sambamba na kutoa misaada ya kibinadamu inayozidi kuongezeka miongoni mwa raia wenye uhitaji ambao nao idadi yao inaongezeka.

3990784

Kishikizo: afghanistan oic taliban
captcha