Kwa mujibu wa taarifa misikiti 3500 kati ya misikiti yote 18,000 Algeria ilifungwa kutokana na janga la corona na bado hakuna sala za jamaa katika misikiti hiyo.
Wizara ya Wakfu ya na Masuala ya Kidini Algeria inasema kufuatia kupungua maambukizi ya corona nchini humo baada ya kutekelezwa sheria za kutotoka nje, misikiti sasa itaanza kutafunguliwa hatua kwa hatua kuelekea katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Maimamu wa misikiti nchini Algeria kwa mara kadhaa sasa wametoa mwito kwa serikali kuruhusu misikiti ifunguliwe tena kufuatia kupungua maambukizi na pia baada ya kuanza zoezi la chanjo ya corona nchini humo.