TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Nizamyie (Nizamiye Masjid) ni msikiti ulioko katika mji wa Midrand, katika Manispaa ya Johanesburg nchini Afrika Kusini.
Msikiti wa Nizamiye umetajwa kuwa msikiti mkubwa zaidi katika Nusufute ya Kusini. Msikiti huo ulianza kujengwa mwaka 2009 na ulikamilika mwaka 2012. Msanifu majengo asili wa msikiti huo alikuwa ni Mturuki na kisha ulijengwa kwa kuzingatia kanuni za ujenzi Afrika Kusini.