IQNA

Ayatullah Makarem Shirazi ampongeza Sheikh wa Al Azhar kwa jitihada za umoja wa Waislamu

21:35 - August 02, 2016
Habari ID: 3470490
Mwanazuoni wa ngazi za juu Iran amempongeza Sheikh Mkuu wa Al Azhar kwa jitihada zake za kuleta umoja wa Waislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ayatullah Makarem Shirazi Marjaa Taqlid wa Kishia nchini Iran ametoa taarifa na kumpongeza Sheikh Ahmed el Tayyib, Sheikhe Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kwa wito wake wa hivi karibuni kwa wanazuoni wa madhehebu za Kiislamu za Shia na Suni kutoa fatwa kwa lengo la kumaliza migogoro ya kimadhehebu miongoni mwa Waislamu.

Hivi karibuni, akijibu swali la tovuti ya Kuwait ya al-Anba kuhusu ulazima wa kukurubisha Waislamu wanaofuata madhehebu za Shia na Sunni, Sheikh el Tayyib alisisitiza kuwa hakuna tafauti baina ya Shia na Sunni kwani wote wanaamini kuhusu Tauhidi na Unabii wa Muhammad SAW.

Ameongeza kuwa Al Azhar inafuatilia suala la kukurubisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni kama stratijia yake muhimu.

Sheikhe mkuu wa al Azhar pia aliwakosoa wale ambao wanalenga kuibua hitilafu na migongano baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni na kubainisha masikitiko yake kuwa watu hawa hawataki kuzima moto wa fitina za kimadhehebu.

Ayatullah Makarem Shirazi amemtaja Sheikh Tayyib kuwa ni mwenye kufahamu ukweli wa mambo katika duniania ya leo. Aidha ameelezea matumaini kuwa wanazuoni wa Shia na Suni watatoa Fatwa ya pamoja dhidi ya misimamo mikali ya kidini na malumbano ya kimadhehebu.

3518860

captcha