IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wanaume Texas Marekani wajifunza kuwapiga risasi Waislamu

17:52 - May 29, 2016
Habari ID: 3470345
Kundi la wanaume jimboni Texas nchini Marekani wanapata mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwaua Waislamu huku wakitumbukiza risasi zao katika damu au mafuta ya nguruwe katika mazoezi hayo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mazoezi hayo ya kikatili yanafanywa na kundi la BAIR la watu wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu na ambalo limeanzishwa kukabiliana na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Amerika (CAIR) pamoja na taasisi zingine zote za kutetea Uislamu.

Mwanachaama mmoja wa kundi hilo lenye misimamo ya kufurutu adha amesikika akisema, anajatayarisha ili kukabiliana na kile ambacho amesema ni 'mwamko' ambao unaweza kuanzishwa na wakimbizi Waislamu katika jimbo hilo.

Kunda video inayowaonyesha wafuasi wa kundi la BAIR wakiwa katika mazoezi ya kufyatua risasi wakitimia aina mbali mbali za bunduki. Wafuasi wa BAIR wanasema wanatumbukiza risasi zao katika damu au mafuta ya nguruwe katika mazoezi hayo ili eti Waislamu watakaouawa kwa raisasa hizo waende motoni.

Chuki dhidi ya Uislamu Marekani imeenea atika miezi ya hivi karibuni hasa katika kampeni za uchaguzi wa rais mwaka huu wa 2016.

Waislamu nchini Marekani, wamesema kuwa maneno ya chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu (Islamophobia) yanayotolewa na viongozi wa chama cha Republican, ndiyo sababu ya kuongezeka hujuma na mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo. Uhasama dhidi ya Waislamu nchini Marekani hasa uliongezeka baada ya Donald Trump, mgombea urais kwa chama cha Republican kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu wakati wa kampeni zake za kuwania uteuzi wa chama chake. Trump ameitaka serikali ya Marekani ipige marufuku kuingia Waislamu nchini humo bila ya kujali wanatokea wapi.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, mashambulio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni mjini Paris Ufaransa, Saint Bernardino, California nchini Marekani na Brussels Ubelgiji yametoa fursa kwa maadui wa Uislamu kupata kisingizio cha kuzidi kuonesha chuki zao dhidi ya Waislamu. Lakini ukweli ni kwamba vitendo vya kigaidi vinavyofanywa kwa jina la Uislamu havina mfungamano wowote na dini hiyo tukufu aliyokuja nayo mja bora kabisa ambaye ni rehema kwa walimwengu wote.

3459946
captcha