Ban ameyasema hayo Ijumaa katika kongamano
kuhusu kuzuia itikadi kali katili linaloendelea mjini Geneva Uswisi ambapo ameiomba
nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono mpango wake wa kupambana na
ugaidi. Ban amesisisitza kwamba ugaidi hauhusiani na dini, kabila au taifa moja
tu, bali unaathiri dunia nzima. Hata hivyo ameongeza kwamba wengi wa waathirika
wa ugaidi ni Waislamu.
Katibu Mkuu amezingatia hatari ya tishio la ugaidi kwa mshikamano wa jamii,
usalama wa kimataifa, na maadili ya Umoja wa mataifa. Amefafanua zaidi mpango
wa Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi, akieelezea kwamba cha msingi ni kuzuia
vitendo hivyo visitokee kwa kukabiliana kwa pamoja na mizizi yake vikiwa ni
pamoja na umaskini, ukosefu wa ajira na mivutano ya kisiasa.
Ameongeza kuwa, "Kuzuia itikadi kali katili kunapitia njia
mbalimbali, lakini dharura zaidi ni kutunza na kuwezesha wavulana na wasichana.
Wao ni wahanga mara mbili: Wanashawishiwa kujiunga na vikundi kali katili na pia
wanashambuliwa kwenye sehemu za burudani, shule na vyuo.”
Kikao cha kimataifa cha kuzuia kuenea vitendo vya uchupaji mipaka mjini Gemeva Uswisi kimehudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri kutoka nchi 30 duniani. Kikao hicho kimefanyika katika hali ambayo kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh katika miezi ya hivi karibuni limetenda jinai chungu nzima katika nchi za eneo hili khususan huko Iraq na Syria kwa kuungwa mkono kifedha na kijeshi na Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu.