IQNA

Arabsat yalaaniwa kwa kuzima Televisheni ya Al Manar

5:26 - December 06, 2015
Habari ID: 3460128
Shirika la Kutoa Huduma za Satalaiti kwa Televisheni limelaaniwa kwa kuzima televisheni ya Al-Manar iliyokuwa ikirusha matangazo yako kupitia mitambo ya shirika hilo.

Jumuiya ya Radio na Televisheni za Palestina imesema hatua ya Arabsat dhidi ya Al-Manar ni katika njama za kuzuia kuenea Intifadha inayoendelea dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Nayo Jumuiya ya Radio na Televisheni za Kiislamu Duniani imelaani hatua hiyo ya kujaribu kuzima sauti ya haki ya Al Manar. Kanali ya Televisheni ya Al Mayadeen, ambayo nayo imefutiwa matangazo yake kupitia Arabsat, imetangaza mshikamano wake na Al-Manar na kutoa wito wa kuanzishwa stratijia mbadala ya vyombo vya habari katika nchi za Kiarabu. Wizara ya Habari ya Syria imelaani vikali hatua hiyo dhidi ya Al-Manar na kusema ushindi unapatikana kwa kueneza haki kama inavyofanya Televisheni ya Al-Manar.
Katika taarifa siku ya Ijumaa, Al-Manar, ambayo inasimamiwa na Harakati ya Hizbullah' ilitangaza rasmi kuwa Arabsat imeamua kuzima matangazo yake. Hatahivyo Al Manar imesema itaendelea kuunga mkono Wapalestina na itakuwa Sauti ya Waarabu na Waislamu wote wanaopambana na dhulma. Shirika la Arabsat lina makao yake Riyadh Saudi Arabia na inaaminika kuwa hatua hiyo dhidi ya Al Manar imechukuliwa kufuatia mashinikizo ya watawala wa ukoo wa Aal Saud.

3459900

captcha