IQNA

Magaidi wa ISIS washambulia Paris, watu zaidi ya 160 wauawa

13:27 - November 14, 2015
Habari ID: 3448027
Watu wasiopungua 160 wameuawa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris Ijumaa usiku katika mashambulizi yanayosadikiwa kuwa makubwa zaidi nchini humo tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti kuwa karibu watu 100 waliokuwa wakishikiliwa mateka wameuawa katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan mjini Paris.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa magaidi walifyatua risasi kwa kipindi cha kati ya dakika 10 hadi 15 katika hujuma hiyo. Maafisa wa serikali ya Ufaransa wanasema gaidi mmoja ameuawa baada ya polisi kuvamia eneo hilo na wengine watatu wamejilipua. Watu wengine katibu 40 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi mengine yaliyotokea kwenye maeneo mbalimbali ya mjini Paris.
Ripoti zinasema watu 200 wamejeruhiwa katika mashambulizi mbalimbali ya jana mjini Paris na kwamba 80 miongoni mwao wako katika hali mahututi
Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameyataja mashambulizi ya jana mjini Paris kuwa ni ya kigaidi yasiyokuwa na mfano.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS au Daesh limetangaza kuwa ndilo lililotekeleza mashambulizi ya jana mjini Paris.
Serikali ya Ufaransa imetangaza hali ya hatari kote nchini humo.
Mashambulizi hayo yamelaaniwa na jamii ya kimataifa na viongozi wa nchi mbalimbali. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeyataja mashambulizi hayo kuwa ni ya kigaidi na kinyama.

Kufuatia hujuma hiyo Rais Hollande wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari kitaifa na kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na kwamba jeshi litatumika kulinda usalama. Hilo ndilo shambulizi baya zaidi katika miaka ya hivi karibuni barani Ulaya.

3447760

captcha