IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah

Israel ni hatari kwa nchi za Kiislamu

16:54 - February 17, 2014
Habari ID: 1376427
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, amekosoa kughafilika kwa nchi za Kiislamu juu ya hatari ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao ni tishio kwa Lebanon, palestina na ulimwengu mzima.

Kwa mujibu wa Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA,Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa, hii leo nchi zote za Kiislamu zinajishughulisha na mambo yao ya ndani, huku zikisahau hatari ya utawala wa Kizayuni. Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo Jumapili usiku katika maadhimisho ya siku ya Shahidi. Sambamba na kuwatukuza mashahidi wa muqawama, Katibu Mkuu wa Hizbullah amezungumzia hali ya nchi za Kiislamu katika eneo hivi sasa na kuitaka Marekani na utawala wa Kizayuni kupata fundisho kwa ushindi wa muqawama na kuongeza kuwa, kile wanachokitaka Washington na Tel Aviv  ni kuliondoa taifa la Palestina kutoka katika  mstari wa mapambano kwa manufaa ya Israel. Akiashiria uwezo mkubwa wa harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan ameuhutubu utawala wa Kizayuni kwa kusema kuwa,  lazima adui afahamu kuwa, uwezo wa Hizbullah uliokuwa ukiogopwa na utawala wa Kizayuni hapo kabla, bado upo pale pale na umezidi kuimarika zaidi. Kwa upande mwingine amezungumzia kadhia ya Syria na kusema kuwa, Saudi Arabia imepigana kwa nguvu zake zote kutaka kuiangusha serikali ya Damascus, lakini  hii leo viongozi wa Riyadh wenyewe wamefahamu kuwa, watakuwa katika hali ngumu baada ya wapiganaji wa Kiwahabi kurejea nchini humo.

1375962

captcha