IQNA

Maadili katika Qur'ani / 9

Mabishano; Njia inayopelekea kupoteza ukweli

17:15 - July 05, 2023
Habari ID: 3477243
TEHRAN (IQNA) – Uislamu unapinga vikali mabishano na majibizano kwa sababu aghalabu ya wanaojihusisha nayo hujichafua kwa chuki na upendeleo, na hulenga kupata ushindi bila kuwa na nia ya kubainisha ukweli.

Mfano mmoja wa vitendo vinavyoficha ukweli na kusaidia uwongo kuwa ushindi ni mabishano. Mazungumzo yanaweza kuwa ya aina mbili. Katika moja, pande hizo mbili hutafuta kupata ukweli na kufuata njia sahihi ya kuufikia.

Kwa upande mwingine, mmoja au pande zote mbili hazijui suala linalojadiliwa na wanataka tu kushinda hoja, na hivyo ili kuhakikisha hoja yao inapata ushindi wako tayari kusema uwongo mwingi. Haya ni mabishano, na Uislamu haukubaliani nayo na hutazamwa kuwa ni dhambi kwa sababu huambatana na chuki na upendeleo na hulenga tu  kupata ushindi na sifa na wala sio kubaini ukweli.

Baadhi ya aya za Qur’ani zinabainisha suala la ugomvi: “ Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika hii Qur'ani kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi. (Aya ya 54 ya Surah Al-Kahf)

Kulingana na aya hii, watu ambao hawajakua kiroho wana uwezekano mkubwa wa kushiriki katika mabishano. Wale wanaokengeuka kutoka kwenye Fitra (maumbile) yao safi hujiingiza katika mizozo, husimama kinyume na ukweli, na hujifungia njia ya uongofu kwao wenyewe, na huu ni msiba mkubwa ambao umewakumba wanadamu katika historia yote.

Tunasoma katika Aya ya 3 ya Surah Al-Hajj: “ Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, na wanamfuata kila shet'ani aliye asi."

 Aya hii inawaelezea wale wanaojihusisha na mabishano kama wafuasi wa shetani. Hii inaonyesha kwamba kugombana kwa nia mbaya ni kukanyaga njia ya Shetani. Kumfafanua shetani kuwa ‘mwasi’ kunaonyesha ukweli kwamba wale wanaohusika katika mabishano wanaasi dhidi ya kweli.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 121 ya Surah Al-Ana’am: “Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina."

Waabudu sanamu walibishana kwamba walikula nyama ya wanyama waliokufa kwa sababu Mungu alikuwa amewaua, na hiyo ni bora kuliko mnyama aliyeuawa na wanadamu.

Uhalali huu usiofaa wa kula nyama ya wanyama waliokufa ndio mashetani kwa sura ya binadamu na majini walivyopendekeza kwa marafiki zao ili wapate kuupinga ukweli. Kwa hivyo mabishano kama haya yana misukumo ya kishetani.

captcha