IQNA

Harakati za Qur'ani

Idhaa ya Qur'ani ya Misri yaadhimisha miaka 60 tokea iasisiwe

20:21 - April 24, 2024
Habari ID: 3478725
IQNA - Sherehe imefanyika katika Radio au Idhaa ya Qur'ani ya Misri huko Cairo kusherehekea kumbukumbu ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa kituo hicho cha redio

Kaulimbiu ya sherehe hiyo ilikuwa  “Idhaa ya Qur'ani; Miaka 60 ya kutumikia Kitabu cha Mwenyezi Mungu."

Ilikuwa ni shukrani ya miaka sitini ya juhudi za wafanyakazi na wasimamizi wa redio kutumikia Kitabu Kitakatifu na kuendeleza mafundisho ya Kiislamu.

Inayojulikana kama idhaa kongwe zaidi ya Qur'ani duniani, imekuwa na jukumu muhimu katika kuongeza ufahamu wa umma kuhusu mafundisho ya kidini nchini Misri.

Vipindi vyake pia vimekuwa maarufu kwa mamilioni ya Waislamu katika nchi zingine.

Idhaa ya Qur'ani ya Misri ilizinduliwa mwishoni mwa Machi 1964. Mara ya kwanza, ilitangaza vipindi saa 14 kwa siku katika sehemu mbili, kuanzia saa 12 asubuhi hadi tano mchana na kisha kutoka nane mchana hadi saa nne usiku

Moja ya vipindi vikuu vya idhaa hiyo likuwa ni qiraa ya visomo vya Qur'ani  vikianza na vile vya Sheikh Mahmoud Khalil al-Husari, qari mkuu wa Misri wakati huo.

Baadaye, ilirusha pia visomo vya Qur'ani vya makari mashuhuri kama Sheikh Mustafa Ismail, Sheikh Muhammad Sidiq Minshawi, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, na Sheikh Mahmoud Ali al-Bina.

captcha