IQNA

Nakala za kale za Qur’ani

17:22 - March 02, 2015
Habari ID: 2917897
Baadhi ya nakala za kale zaidi za Qur’ani duniani ambazo ni zama miaka ya awali ya Uislamu zimewekwa katika maonyesho.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, baadhi ya nakala hizo ziko nchini Ujerumani, Uturuki, Misri, Uingereza na Yemen.  Nakala hizo ni ishara kuwa Kitabu Kitakatifu cha Waislamu, kinyume na vitabu vya dini nyinginezo, kimehifadhika pasina kuwepo mabadiliko yoyote tokea ateremshiwe Wahy Mtume Muhammad SAW zaidi ya miaka 1,400 iliyopita.


Kati ya nakala hizo tunaweza kuashiria zifuazo:
1) Nakala ya Qur’ani ya kati ya mwaka 649—674 Miladia. Nakala hiyo ilipatikana mwezi Novemba mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Tubingen Ujerumani. Wataalamu waliochunguza nakala hiyo wanasema wana uhakika wa asilimia 95 kuhusu tarehe yake.


2) Nakala nyingine ni ile ya takribani miaka 200 hadi 300 baada ya Hijra (karne za 9-11 Miladia). Nakala hii ya msahafu ina kurasa 536 na imepatikana katika eneo la Dong Xiang kusini magharibi mwa China.


3) Nakala nyingine ni ile inayokadiriwa kuandikwa miaka 200-600 baada ya Hijra nayo ilipatikana kusini magharibi mwa China na inahifadhiwa katika Msikiti wa Tsih Jih nchini humo.


4) Nakala ya nne ni ile inayokadiriwa kuandikwa karne 12 zilizopita na iligunduliwa mwaka 2013 na Imamu wa  msikiti katika eneo la Bodrum Uturuki. Msahafu huo sasa umehifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Izmir nchini Uturuki.


5) Nakala nyingine ni ile ijulikanayo kama ‘Nakala ya Uthmaniya’. Inadokezwa kuwa iliandikwa katika zama za Ukhalifa wa Uthmaniya na imehifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Telyashayak nchini Uturuki. Msahafu huo wenye kurasa 1087 una uzito wa kilo 80.
6) Nakala nyingine ya msahafu wa kale ni ile iliyopewa jina la Qur’ani ya Ma’il. Baadhi ya Wanahistoria wanaamini kuwa iliandikwa karne ya 8 Miladia katika mji mtakatifu wa Makka au Madina. Tokea karne ya 19 miladia nakala hiyo ya Qur’ani inahifadhiwa na katika Jumba la Makumbusho la Uingereza.


7) Nakala ya saba ni ile inayokadiriwa kuandikwa  mwaka 650 hadi 675 Miladia na imeandikwa katika ngozi ya kondoo. Iligundiliwa katika Msikiti wa Amr eneo la Fustat nje kidogo ya mji wa Cairo Misri. Baadhi ya kurasa za msahafu huo zimehifadhiwa katika Jumba la Kitaifa la Makumbusho Ufaransa.
8) Nchini Yemen kumepatikana nakala ya Qur’ani ya mwaka 200 Hijria. Nakala hiyo ilipatikana mwaka 2012 katika pango mjini Ad Dali nchini humo.
9) Nakala nyingine ilipatikana katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a na iliandikwa katika miongo miwili ya awali ya karne ya nane Hijria.../mh

2917585

captcha