IQNA

Msikiti wa 7 kwa ukubwa duniani wafunguliwa Pakistan

21:36 - October 12, 2014
Habari ID: 1459697
Msikiti wa saba kwa ukubwa zaidi duniani umefunguliwa katika mji wa Lahore nchini Pakistan.

“Msikiti huu utakuwa nembo ya Pakistan kote katika ulimwengu wa Kiislamu”, amesema meya wa eneo la Bahria Malik  Riaz.
Msikiti huo ujulikanao kama Masjid Jamia Bahria ulifunguliwa na Rais Yusuf Ali Zardari wa Pakistan kwa mnasaba wa Siku Kuu ya Idul Adha. Msikiti huo una uwezo wa kubeba waumini 70,000 huku 25,000 wakiwa ndani ya ukumbi mkuu wa msikiti. Msikiti huo wa Jamia  ulio na kuba 21 na minara yenye urefu wa fiti 165 umetambuliwa kama  msikiti wa saba kwa ukubwa duniani huku ukiwa ndio mkubwa zaidi duniani.
Ghorofa ya pili ya msikiti huo ni maalumu kwa wanawake waumini na usanifu majengo wake umetajwa kuwa wenye kupatailhamu kutoka mtindo ya Mughal...mh/
1458955

captcha