IQNA

Tarjama ya Kiswahili ya Nahjul Balagha yachapishwa Tanzania

15:28 - June 30, 2014
2
Habari ID: 1424341
Tarjama ya Kiswahili ya Nah-ul-Balagha imechapishwa kwa mara ya kwanza kwa hisani ya Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA  Afrika Mashariki, tarjama hiyo  imechukua miaka saba kutayarishwa na imechapishwa na taasisi ya Al-Itrah Foundation yenye makao yake mjini Dar-es-Salaam.
Mtarjumi wa Nahj-ul-Balagha kwa lugha ya Kiswahili ni mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Tanzania Sheikh Harun Pingili ambaye ameitarjumu kwa Kiswahili kutoka Kiarabu.
Nahj-ul-Balagha  ni majmua ya khutba, barua, risala, mawaidha na semi za Amirul Muuminin Ali Bin Abu Talib AS. Majmua hiyo ilikisanywa na al-Sharif al-Radhii, mwanazuoni wa Kisia wa karne ya 10. Mbali na faida na thamani yake kubwa ya kidini, Nahj-ul-Balagha pia inasifika kwa umahiri wake wa kifasihi.
1423462

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Baaqir Kitenge
0
0
Iwekeni online mfumo wa Pdf ili tuweze kuipata kirahisi kwa kudownload
nasma halidi
0
0
nikitabu kizur ambacho kina toa elimu ya kila siku kipitia imam ali a.s
captcha