IQNA

Hija ndogo ya Umrah

Saudi Arabia yaongeza Muda wa Visa ya Umrah hadi Miezi 3

23:39 - October 03, 2022
Habari ID: 3475875
TEHRAN (IQNA) – Mamlaka ya Saudia inasema visa ya Hija Ndogo ya Umrah imeongezwa kutoka mwezi mmoja hadi mitatu kwa mataifa yote.

Haya yalitangazwa na Waziri wa Hajj na Umrah Tawfiq Al-Rabiah Jumapili.

Tangazo hilo linakuja chini ya wiki moja baada ya Saudi Arabia kusema jukwaa jipya la "nusuk.sa" litakuwa lango kuu la kutembelea miji mitakatifu.

"Nusuk.sa" inawawezesha wale wanaotaka kutekeleza Umra au kutembelea kupata visa na vibali vinavyohitajika, na kulipia safari njia ya kielektroniki.

Huduma zingine mbalimbali zitatolewa baadaye, ikiwa ni pamoja na ramani shirikishi, mwongozo wa kidijitali wa maagizo yote katika lugha kadhaa, na maelezo ya afya.

Hija Ndogo ya Umrah ilianza tena katika siku ya kwanza ya mwezi wa Hijri wa Muharram, ambayo iliangukia tarehe 30 Julai.

Umra ni safari ya kwenda Mecca ambayo Waislamu wanaweza kuitekeleza wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hijja ambayo inaweza kufanywa tu katika siku za kwanza za mwezi wa Hijri  Qamari wa Dhul Hajja.

Mwaka huu, mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali walishiriki katika ibada ya Hija.

Msimu wa Hajj ulianza Julai 1, ukiashiria msimu wa kwanza wa hija baada ya janga baada ya miaka miwili ya usumbufu mkubwa uliosababishwa na COVID-19.

3480705

Kishikizo: umrah saudi arabia
captcha