IQNA

Msomi wa Iraq: Vyombo vya habari vihimiza umoja wa Kiislamu

18:44 - October 23, 2021
Habari ID: 3474461
TEHRAN (IQNA)- Vyombo vya habari vya ulimwengu wa Kiislamu vinapaswa kuimarisha jitiahda zaidi kustawisha umoja wa Kiislamu, amesema msomi wa Iraq.

Akizungumza na IQNA kwa mnasaba wa Wiki ya Umoja wa Kiislamu, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Baghdad, Profesa Hisam al Jabouri amesema vyombo vya habari  katika ulimwengu wa Kiislamu vimeonyesha utendaji dhaifu katika Nyanja mbali mbali ikiwemo Nyanja ya umoja wa Kiislamu.

Amesema moja ya sababu hiyo ni kuwa idadi kubwa ya vyombo vya habari vinafadhiliwa na serikali ambazo aghalabu hufadhiliwa na serikali na hivyo hujikita zaidi katika kusimu mifumo fisadi na dhaifu ya kisiasa huku vyombo vingine vya habari vikijikita katika kueneza itikadi zisizo za kidini.

Al Jabouri amesema ulimwengu wa Kiislamu unahitaji vyombo vya habari ambavyo vinafungamana na misingi ya kuhimiza umoja wa Kiislamu.

Aidha amesema mitandao ya kijamii na intaneti inaweza kutumika vivuri kwa ajili ya kuwakurubisha Waislamu wa maeneo mbali mbali duniani.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal.

Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu.

4003742

captcha