IQNA

Sisizito la mafunzo ya ufahamu wa Qur'ani katika shule nchini Sudan

22:46 - August 04, 2021
Habari ID: 3474158
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Wakfu nchini Sudan amesisitiza umuhimu wa kufundisha sayansi ya dini na ufahamu wa Qur'ani shuleni.

Nasruddin Mufarrah, Waziri wa Wakfu Sudan, ambaye alikuwa akizungumza katika hafla iliyofanyika kuwaenzo waliohifadhi Qur’ani Tukufu mjini Cairo, Misri pia aliangazia umuhimu wa kutafakari kuhusu mafundisho ya  Qur'ani na kujifunza fadhila za Qur'ani.

Kikao hicho kilifanyika  mnamo Agosti 3 ili kuwaenzi waliohifadhi Qur’ani katika  Jumuiya ya Wanaohifadhi Qur’ani katika Idara ya Mahakama Misri.

Kikao hicho kilifanyika kwa ushiriki wa Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Wakfu wa Misri, Sheikh Ahmad Umar Hashem, rais wa zamani wa Al-Azhar na mjumbe wa Baraza Kuu la Wasomi wa Al-Azhar, Osama Al-Azhari, mshauri wa rais wa Misri katika dini mambo, Nasruddin Mufarrah, Waziri wa Wakfu na Maswala ya Kidini wa Sudan na Muhammad Elyas Al-Haj, balozi wa Sudan nchini Misri.

3988408

Kishikizo: sudan qurani tukufu
captcha