IQNA

Muirani wa kwanza kushinda medali ya dhahabu Mchezo ya Olimpiki Tokyo 2020

19:55 - July 25, 2021
Habari ID: 3474125
TEHRAN (IQNA)- Javad Foroughi, 41, muuguzi katika Hospitali ya Baqiyatullah mjini Tehran amekuwa Muirani wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Foroughi ni baba mkarimu ambaye hutumia wakati wake mwingi kusoma Qur’ani na hivyo amewezea kupata sifa ya ukarimu.

Mke wake na watoto wake nao pia humfuata katika kuhakikisha maisha yao yanaenda sambambamba na mafundisho ya Qur’ani Tukufu kama ambavyo pia wagonjwa anaowahudumia hunufaika pia na ucha Mungu wake.

Muuguzi huyo maarufu wa Iran ameweka historia katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 baada ya kupta medali ya dhahahbu jana katika mashindano ya kulenga shabaha kwa bunduki umbali wa mita 10 shindano la wanaume. Punde baada ya kushinda medali hiyo, Froughi alisujudu na kumshukuru Allah SWT kwa taufiki aliyopata.

Hii ni medali ya kwanza ya Iran katika shindano ya kulenga shabaha kwa bunduki katika Olimpiki.

 
 
captcha