IQNA

Mauaji ya watu asili wa Canada, dosari kubwa katika Kanisa Katoliki

22:07 - June 27, 2021
Habari ID: 3474047
TEHRAN (IQNA)- Kugunduliwa makaburi ya mamia ya watoto wa Wacanada asili waliokuwa wakishikiliwa kwa lazima katika shule za wamishonari wa Kikatoliki kumezua wimbi kubwa la hasira kati ya raia wengi wa nchi hiyo, taasisi za kutetea haki za binadamu na baina ya wapenda haki kote duniani.

Kugunduliwa kwa mabakuri hayo ya watoto ni ushahidi madhubuti wa ubaguzi wa rangi na wa kimbari katika nchi za Magharibi hususan Canada na Marekani, na sasa kumewafanya wenyeji asili wa Canada wamtake Rais wa Marekani, Joe Biden afanye uchunguzi kuhusu hatima ya watoto wa jamii hiyo huko Marekani. Boby Cameron ambaye ni Mwenyekiti wa Federesheni Mataifa Huru ya Wenyeji wa Wakazi Asili amemwambia Rais wa Marekani kwamba: "Serikali ya Washington pia inawajibika kufanya uchunguzi kuhusu shule za wakazi asili katika miaka iliyopita kwa sababu katika nchi yako pia kuna makaburi mengi sana ambayo hayakuwekewa alama yoyote." 

Mshtuko Canada

Uchunguzi wa kutafuta makaburi ya umati ya wakazi asili wa Canada ulianza mwishoni mwa mwezi Mei baada ya kugunduliwa mabaki ya maiti 215 za wanafunzi wa shule ya bweni ya Kikatoliki ya Kamloops Indian katika jimbo la British Columbia iliyofungwa mnamo 1978. Baada ya hapo Alkhamisi wiki hii mtandao wa gazeti la The National Post la Canada uliripoti kwamba, kumegunduliwa mamia ya makaburi ambayo hayajasajiliwa katika mkoa wa Saskatchewan ambayo inadhaniwa yana maiti za watoto waliokuwa wakishikiliwa katika shule nyingine ya bweni ya wamishonari wa Kikatoliki. Makaburi hayo ambayo hayana alama yoyote yana maiti za watoto 751. Kugunduliwa makaburi haya kumezusha mshtuko mkubwa nchini Canada na maeneo mengine ya dunia. Kwa sasa zinafanyika jitihada za kusaka makaburi mengine ya aina hiyo.  

نسل‌کشی بومیان کانادا؛ لکه ننگ ابدی بر دامن کلیسای کاتولیک

Rosanne Casimir ambaye ni mkuu wa mojawapo ya makabila ya mji wa Kamloops katika jimbo la British Columbia amesema baada ya kugunduliwa makaburi hayo kwamba: "Vifo vya watoto hao wa wakazi asilia wa Canada havikusajiliwa katika waraka wowote wa shule, na suala hili peke yake ni ushahidi kwamba, maafisa na viongozi wa shule hizo walihusika katika vifo vya watoto hao."

"Mauaji ya Kimbari ya Kiutamaduni"

Kuanzia mwaka 1883 hadi 1996 zaidi ya watoto laki moja na nusu wa wakazi asili wa Canada walilazimishwa kuishi katika shule makhsusi zilizokuwa zikisimamiwa na wamishonari na wahubiri wa Kikatoliki ili eti kuwaingiza katika jamii ya Canada. Kwa mujibu wa ripoti ya Kamisheni ya Ukweli na Maridhiano ya Canada iliyotolewa mwaka 2015 juu ya kile ilichokiita "Mauaji ya Kimbari ya Kiutamaduni", watoto hao walikabiliana na sulubu na unyanyasaji wa kutisha wa kimwili, ubakaji, utapiamlo na unyama mwingine uliowapata watoto wengi anokadiriwa kuwa zaidi ya 150,000 waliokuwa katika shule hizo, ambazo zilikuwa zikiendeshwa na makanisa ya Kikatoliki kwa niaba ya serikali ya Ottawa. Watoto hao walishikiliwa katika shule hizo kwa shabaha eti ya kuwaingiza kwenye utamaduni wa waliowengi. Maelfu ya watoto walionyanyaswa katika shule hizo walipoteza maisha. Viongozi wa jamii za Wacanada asilia wanasema, kugunduliwa makaburi mapya ya watoto wa wenyeji kunatonesha kidonda cha miaka iliyopita.

Si jambo jipya

Alaa kulli, suala la ubaguzi wa rangi na kimbari katika nchi za Magharibi hususan Canada na Marekani si jambo jipya. Historia ya nchi hizo inaambatana sana na ukatili, unyanyasaji na mateso waliyopewa wakazi asilia wa nchi hizo na hasa hasa watu weusi wenye asili ya Afrika. Nchi hizo za Magharibi katika miaka ya karibuni zimekuwa zikijinadi kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu lakini kivitendo zinaendeleza ubaguzi wa kimfumo na unyanyasaji unaolenga raia za jamii za waliowachache, wahajiri na wakimbizi. Hali hiyo imekuwa mbaya zaidi huko Magharibi katika kipindi cha sasa cha maambukizi ya virusi vya corona. Ubaguzi na manyanyaso hayo katika kipindi cha sasa unadhihirika zaidi kwa kunyanyapaliwa wakazi asili na raia wenye asili ya Afrika wakati wa kugawa chanjo za corona na madawa ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

نسل‌کشی بومیان کانادا؛ لکه ننگ ابدی بر دامن کلیسای کاتولیک

Fidia

Nchini Canada wakazi asili wa nchi hiyo wanasumbuliwa na mambo mengi ya kimingi ikiwa ni pamoja na kukosa huduma ya maji safi. Gazeti la Guardiani limeandika kuwa, viongozi wa wakazi asili wa Canada wameifungulia mashtaka Serikali ya Federali ya nchi hiyo na kudai fidia kutokana na kunyimwa huduma ya maji safi katika nchi ambayo ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa zaidi wa vyanzo vya maji safi duniani.  

Sasa maudhui ya mauaji ya watoto wa wakazi asili wa Canada imevuka mpaka ya kuingia nchi jirani ya Marekani kwa kadiri kwamba, utafiti uliofanyika umeonesha kuwa, yumkini baadhi ya watoto hao walihamishiwa Marekani. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana Mwenyekiti wa Federesheni ya Mataifa Huru ya Wakazi Asili akasema, kuna makaburi mengi sana yasiyo na alama nchini Marekani na amemtaka rais wa nchi hiyo kushirikiana na viongozi wa wenyeji hao katika suala hilo.        

3980265

captcha