IQNA

Wizara ya Afya ya Iran yaweka sheria za maombolezo ya Mwezi wa Muharram

19:49 - August 04, 2020
Habari ID: 3473032
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Afya ya Iran imetangaza maelekezo ya kiafya ambayo yanapaswa kufuatwa katika wa maombolezo ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.

Naibu Waziri wa Afya wa Iran Ali Reza Raisian amesema hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na waumini kutokaribiana ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Aidha watakaodhuhuria maombolezo katika mwezi wa Muharram watalazimika kuvaa barakoa huku wazee na wenye magonjwa sugu wakitakiwa waomboleze wakiwa majumbani.

Ugonjwa wa corona uliibuka mara ya kwanza mjini Wuhan, China Disemba mwaka jana na sasa umeenea kote duniani ambapo watu zaidi ya milioni 18.4 wameambukizwa na wengine wasiopungua 680 wamepoteza maisha. Ugonjwa wa corona umevuruga sekta zote duniani ziwe za kidini, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo.

3914551

captcha