IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah

Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS yamewaingiza maadui kiwewe na wahka

21:55 - October 19, 2019
Habari ID: 3472179
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, uwepo wa mamilioni ya watu mjini Karbala ni jambo lisilo na mfano katika historia na kwamba Marekani, utawala haramu wa Kizayuni, mabeberu na madhalimu wa dunia wanahisi hofu kubwa kwa kushuhudia matembezi ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya Imam Hussein AS

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo Jumamosi mchana katika mji wa Baalbek kwa mnasaba wa marasimu ya Arubaini ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS na kuongeza kuwa, uwepo wa mamilioni ya watu katika marasimu hayo hauna mfanano duniani ambapo watu kutoka maeneo yote ya dunia ikiwemo Ulaya na Marekani wamefika Karbala kwa lengo hilo. Ameongeza kuwa matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS kwa mara nyingine yamewadhihirishia wazi walimwengu hamasa ya mjukuu huyo wa Mtume.

Aidha Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon sambamba na kuashiria matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon amesema kuwa, baadhi ya viongozi serikalini na katika makundi ya kisiasa wanataka kukwepa majukumu yao na kujiweka kando sambamba na kuwatwisha wengine matukio ya sasa, suala linaloonyesha kutokuwepo mshikamano wa kitaifa na kutojali matukufu ya kiakhlaqi na kibinaadamu katika kushughulikia mustakbali wa wananchi.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuwa, ni lazima Walebanon washirikiane ili kuboresha uchumi na hali ya wananchi. Ameongeza kuwa mambo kama vile kutaka kufanyike uchaguzi wa bunge wa kabla ya wakati na kuundwa serikali mpya ni yenye kupoteza muda na kwamba serikali ya sasa ni lazima iendeleze shughuli zake kwa utaratibu mpya sambamba na kupata ibra kutokana na malalamiko ya hivi karibuni ya wananchi. Aidha Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amewahutubu waandamanaji kwa kusema kwamba, Hizbullah inaheshimu sauti na malalamiko yao hivyo muqawama, hautaiacha nchi na taifa la Lebanon kama ambavyo hautaruhusu Lebanon ipate madhara.

3850893

captcha