IQNA

Maonyesho ya historia ya uchapishaji Qur'ani nchini Algeria

10:58 - April 02, 2019
Habari ID: 3471896
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho ya historia ya uchapishaji Qur'ani Tukufu yanafanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo ya siku nne yalianza Jumatatu na yameandalia na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini nchini humo.
Wanaotembelea maonyesho hayo wanapata fursa ya kujifunza historia ya uchapishaji Qur'ani nchini Algeria mbali na kuona nakala za kale za Qur'ani.
Halikadhalika maonyesho hayo yanaonyesha mbinu za kale ambazo zilikuwa zikitumika kufunza kuhifadhi Qur'ani nchini humo.
Pembizoni mwa maonyesho hayo kuna warsha za kuwafunza washiriki misingi ya kaligrafia ya Kiarabu.
Algeria ni nchi ya Kiislamu iliyoko kaskazini mwa Afrika na asilimia 99 ya wakazi wake ni Waislamu.

3800449

captcha